Mtakatifu wa Siku ya Februari 23: Mtakatifu Polycarp
Hadithi ya Mtakatifu Polycarp: Polycarp, askofu wa Smirna, mfuasi wa Mtakatifu Yohana Mtume na rafiki wa Mtakatifu Ignatius wa Antiokia, alikuwa kiongozi wa Kikristo aliyeheshimika katika nusu ya kwanza ya karne ya pili.
Mtakatifu Ignatius, akiwa njiani kwenda Roma ili kuuawa kishahidi, alimtembelea Polycarp huko Smirna, na baadaye huko Troa alimwandikia barua ya kibinafsi.
Makanisa ya Asia Ndogo yalitambua uongozi wa Polycarp kwa kumchagua kama mwakilishi wa kujadili na Papa Anicetus tarehe ya sherehe ya Pasaka huko Roma-mabishano makubwa katika Kanisa la kwanza.
Barua moja tu kati ya nyingi zilizoandikwa na Polycarp imehifadhiwa, ile aliyoandika kwa Kanisa la Filipi huko Makedonia.
Akiwa na umri wa miaka 86, Polycarp aliongozwa katika uwanja wa michezo wa Smirna uliojaa watu kuchomwa moto akiwa hai
Moto haukumdhuru na hatimaye aliuawa kwa panga.
Jemadari aliamuru mwili wa mtakatifu uchomwe.
“Matendo” ya kifo cha imani ya Polycarp ndiyo masimulizi ya mapema zaidi yaliyohifadhiwa, yenye kutegemeka kikamili ya kifo cha shahidi Mkristo.
Alikufa mnamo 155.
Soma Pia
Mtakatifu wa Siku ya Februari 22: Mtakatifu Margaret wa Cortona
Ujumbe wa Papa Francis kwa Kwaresima 2023
Papa Francisko Barani Afrika, Misa Nchini Kongo na Pendekezo la Wakristo: "Boboto", Amani
DR Congo: Bomu Lalipuka Kanisani, Takriban watu 17 wameuawa na 20 kujeruhiwa
DR Congo, Walikuwa Wakiandaa Maandamano ya Amani: Wanawake Wawili Watekwa nyara Kivu Kusini